Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Bure ni GHALI Binti MASALAKULANGWA!

>> Thursday, September 08, 2011

 Tatizo la GHARAMA,...
.... labda ni pale  WATU wajisahaupo  kwa  kutostukia KIPIMOcha gharama ni nini,...
.... kitu kifanyacho wasiolipia kwa PESA na waaminio kipimo cha GHARAMA ni PESA kudhania walichokipata wamekipata BURE!

Swali kwako:
  • SI unajua baadhi ya kipimo kigharama ni UTU wako  kitu kifanyacho ukikaa uchi hadharani  labda ni UTU wako  ndio uathirikao KIGHARAMA ingawa  ulikaa uchi BURE kipesa aka hukulipia katika kufanya  watu wakupige chabo maeneo?


Swali kiduchu kwa MASALAKULANGWA :

  • Kwa MHESHIMIWA kidume  MASALAKULANGWA,...
.....unakumbuka kuwa tatizo la GHARAMA watu hujisahau kwa kutumia kipimo cha PESA,...
..... na kama  kitu hakilipiwi kwa pesa wanafikiri wamekipata BURE,...
..... kitu kifanyacho  unaweza kujikuta ingawa HUKULIPIA KUGAWIWA ila unalipia dawa za kutibu GONO, kaswende na zile za kulea  VIJIRUSI vya UKIMWI  visipitilize na kugeuka ugonjwa kamili wa UKIMWI?


Ndio,...
.... labda BURE ni GHALI,...
........ na wakati unastukia unapewa vya bure,...
..... labda stukia pia kuwa labda hiyo sio BURE kwa kuwa gharama zake  labda zimekaa mkao tofauti,...
.... na kama unabisha  muulize Rais Kikwete  jinsi suti za bure  za tajiri wa KEMPISKY zinavyokuwa ghali ghafla kistaili ya WANANCHI kufikiria ALIHONGWA akahongeka ,...
.... hata kama  katika hilo wala hakuna UKWELI!

Swali:
  • SI unakumbuka labda hakuna cha bure DUNIANI kama kipimo  hakita kuwa ni PESA tu hasa ukifikiria  kuna wapewao mpaka MAPENZI  bure ila baadaye kujastukia WANALIPIA kwa kuogopa kuumizwa MOYO/roho na LIMPENZI?

Ndio,...
.... nakubali lakini kuwa,...
.... wakati unafikiria unapata cha bure hasa kama wewe ni mbahiri kidogo au UMECHACHA,...
....vya BURE ni VITAMU aisee,...
.......mpaka pale  tu ustukie unalipia WAPI na KIVIPI.:-(


Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!


Hebu Tshala Muana apenyeze-DEZO DEZO



Au hebu tu tena ABETI MASIKINI atulize kwatamutamu-LIKAYABO




Au tu ABETI MASIKINI aje na kaka yake Aboumba Masikini tena katika ile kitu live waliyofanya Kinshasa mwaka 1974 ya ndude-MIWELA



2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Goodman Manyanya Phiri 2:38 am  

Kataa, kata-kata, Mkuu Simon kupewa vya bure... hata ukipewa na mama yako: mpe chochote kumshukuru.

Simon Kitururu 3:30 pm  

Kweli kabisa Mkuu GOODMAN!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP