Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kwa kuwa katika HATUA aelekeaye SEBULENI huweza kupitia pia CHOONI!

>> Tuesday, September 06, 2011

Kuna wasahauo kuwa kama MTU anafanyia kazi kuelekea SEBULENI,...

...... safari hiyo inategemea tu na mahali alikoanzia na ramani yenyewe kwa kuwa kuna ambao MTU huwakuta nje ya CHOO lakini haina maana kwa kuwa wako mbele ya CHOO basi ndio maanayake hawaelekei SEBULENI!:-(

Swali:
  • Si unajua hata safari ya kuelekea kwenye MAFANIKIO haimaanishi ukiwa umeianza tu itaonyesha unaelekea kwenye MAFANIKIO?

Ndio,...
..... labda waache WASIOFANIKIWA lakini ni wahangaikiao MAFANIKIO wahangaikie tu MAFANIKIO hata usipoona ni penye uhusiano na KUFANIKIWA ,...
.... kwa kuwa katika safari za KUFANIKIWA wengi hukatizia kusiko na DALILI za WATAKAYOFANIKISHA ,...
.... na kuwahukumu wakiwa njiani au CHOONI hakuna ushahidi kuwa ni kweli hapo walipo bado hawaelekei SEBULENI kwenye UBWABWA.:-(

NI wazo tu hili MHESHIMIWA!
Jumanne NJEMA!


Hebu twende tena Cape Verde ili Suzanna Lubrano aanzishe upya kwa miondoko ya Zouk katika -Nha Sonho




Tubaki hapahapa Cape Verde ili tugawiwe muziki aina ya Funana kutoka kwa Som di Terra katika kitu - Mi Nca Burro Nau



Tugewe zaidi miondoko ya Funana kutoka kwa Ferro Gaita katika ndude-Sabe Dimas




Ferro Gaita waje live kwa - É si prôpi


Au turudi tu Ivory Coast ili Magic System wamalizie tu tena kwa-Zouglou Dance


2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 4:44 pm  

Mafanikio:-) Jumanne njema nawe pia Simon!

Simon Kitururu 1:15 am  

@Asante Mtoto Mzuri Yasinta ! Na wewe pia ubarikiwe!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP