Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Siri ya UJINGA wa UPROFESA wa baadhi - LABDA ni ELIMU ZAO.:-(

>> Monday, September 05, 2011

Na  labda,...
.... bado ni kweli kuwa kutafuta ELIMU kwa karibu kila MTU,...
.... ni aina tu mojawapo ya kukiri kiaina kuna kitu MTU hajui na katika hilo LABDA  ,...
.... kuna  KUKIRI kaujianga ndani ya MSOMI huyo ambako kalijificha na utafutaji ELIMU unakafunua chupi!:-(

Swali:

  • Kwani unafikiri wakati MTU anaelimika apatacho ni ELIMU tu?
  • Lakini si INADAIWA akiriye UJINGA huyo kashatatua kipengele kikubwa cha ujenzi wa msingi wa swala la nini ANATAKA KUJUA kimkao wa kujifunza na hilo huweza kumgeuza mwanafunzi wa KUDOKOA kuwa MWIZI hata wa VIDUDE vya WAKE au WAUME wa WATU kimadhubuti na katika hilo akawa KAKUBUHU kiuwalimu?

Ndio,...
.... bado labda kuna UKWELI,...
....... hakuna zuri lisilo kuja na baya lake kiaina hata kama zuri hilo kwa MTU ni ELIMU ,...
...... na  NDIO wakati  MLEVI anajifunza kulewa labda kuna ajifunzalo pia ambalo MLOKOLE hajifunzi MSIKITINI kielimu!:-(


Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(










Hebu turudi tena COLUMBIA ili Choc Quib Town waanzishe upya kwa - El Bombo



Au tu hebu CHOC QUIB TOWN wabadili  gia na KUINGIZA upya hiihii ndude -El Bombo




Manu Chao aingilie tena shughuli kwa- BONGO BONG



Kabla Q-TIP hajabadili mchezo mzima  akirudi na kundi zima la TRIBE CALLED QUEST katika kipele-Can I kick IT




A Tribe called Quest watekenye zaidi kipengele kwa kuongelea - Find a Way




Au jikumbushe TRIBE CALLED QUEST wakija na BUSTA RHYMES katika-OH MY GOD




Au tu TRIBE CALLED QUEST wamalizie ,..
............kwa ndude iliyotuna ile-Bonita Applebum

8 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

sam mbogo 10:22 am  

Mambo ya ujinga kazikwelikweli!!
kaka S

Simon Kitururu 10:27 am  

@Kaka S: Si utani aisee! Na KIUJINGA kuna mpaka MAPROFESA aisee!

Yasinta Ngonyani 11:43 am  

Lakini kumbuka Maprofesa nao ni watu pia.

sam mbogo 11:44 am  

ndiyo maana,sikuhizi katika ujinga huohuo,mtu mbabaishaji,misheni tauni,huitwa MSANII ,inanikera! lakini basi tu,niujinga mtupu kufananisha ,kazi ya mtu ,kama kielelezo cha utapeli,ubabaishaji,wakati mwingine unashindwa kujitambulisha kwa kiswahili kuwa wewe ni msanii? labda uweke kwenye kimombo kidogo,ARTIST.kama usemavyo kwa kusoma /kielimu,profesa si mchezo,lakini inapotokea profesa huyo akawa na kaujinga,tofauti naulivyo m tegemea ,si ajabu ujinga huo si lazima uende shule,ila wakati mwingine ni vyema kuushitukia. wengi hatushitukiagi mambo fulanifulani,ya kidunia na maisha kwa ujumla namatokeo yake twa weza kuitwa wajinga!!, kazi nzuri mtakatifu. kaka S

Simon Kitururu 12:10 pm  

@Kaka S:Na kikubwa kuna waaminio kwa kuwa Profes Sarungi ni Profesa wa MIFUPA basi kila kitu anajua katika levo ya UPROFESA wa MIFUPA.:-(



Na nikweli USANII ni tusi siku hizi wakati WASANII ndio mboge la JICHO kwenye jamii ambapo wakidharaulika labda yote ya jamii kirahisi yatadharaulika!:-(


Asante sana KAKA S kwa kutonitenga hapa KIJIWENI!

Simon Kitururu 12:13 pm  

@Mtoto mzuri Yasinta: Unauhakika NYAU hawana MAPROFESA wao? SI unajua BINADAMU wanamchezo wakudharau viumbe vingine ingawa NDEGE wanawashinda hata kwa kusafiri bila kutumia ramani kutoka ulaya kwenda mpaka AFRIKA na kurudi bila kutumia PASSPORT wa la ndege -bila kusahau labda hata sisismizi na mende wana wajuayo zaidi yafanyayo wastukie kiporo kiko wapi pale WANADAMU wawaitapo JIKONI?

Yasinta Ngonyani 12:30 pm  

Duh! huwa sikubali kushiundwa lakini hapa umeniweza umesema ukweli kabisa mpaka umenifanya nitamani kuwa ndege ...kwani mtu natamani kweli kumwona lakini....kazi nzuri Mtakatifu:-

Simon Kitururu 12:36 pm  

@Da Yasinta: Tuko Pamoja!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP