Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Wawakilishi wa Tanzania katika Bunge La Vijana London

>> Thursday, September 08, 2011

Salam,


Ubalozi wetu wa Tanzania Hapa Nchini Uingereza Kwa Kushirikiana na Ofisi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania wamewateua Linda Kapinga na Lucy Minde ili kwenda kutuwakilisha katika mkutano wa nne wa Commonwealth Youth Parliament ( Bunge la Vijana) ulioanza tarehe 6-10 Septemba 2011 jijini London. Mkutano huu Umeandaliwa na Commonwealth Parliamentary Association tawi la Uingereza ikishirikishwa na Sekretarieti ya CPA ambayo ni Umoja wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola. Katibu wake ni Mwafrika wa kwanza kuteuliwa na Pia ni  Mtanzania mwenzetu  Dr William Shija.  

Lengo kuu la mkutano huu ni kuwawezesha vijana kati ya miaka 19-29 kwa kuwapatia uzoefu wa shughuli za Bunge hasa katika kuimarisha demokrasia ya mabunge na Uchumi. Motto wa Mkutano wa mwaka huu "MABADILIKO YA HALI YA HEWA"

Ubalozi wa Tanzania hapa Uingereza unapenda kuwapongeza sana Linda Kapinga na Lucy Minde kwa kuchaguliwa kwao na pia kuwatakia kila la kheri katika kutuwakilisha kwenye mkutano huu.

Asanteni,
Urban Pulse ikishirikiana Miss Jestina Blog ,...
.........na Ubalozi wa Tanzania UK

Urban Pulse Na Miss Jestina wakifanya mahojiano na Linda

Kushoto Lucy na Linda katika picha ya pamoja Ubalozini

Linda Kapinga mteuliwa mmojawapo

Lucy Akitoa Ufafanuzi wakati wa mahojiano

Lucy Minde Mteuliwa wa Pili

Mh Naibu Balozi katika picha ya pamoja Lucy na Linda walioteuliwa kutuwakilisha katika Bunge la vijana

MH Naibu balozi kwenye picha ya Pamoja akiwa na baadhi ya maofisa wa ubalozi, TMK na mapromota wao waliokuja kuwaunga mkono

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP